Header Ads

DPP:FELESHI: TUNATOA HAKI SI KUFUNGA WATU



DPP:FELESHI TUNATOA HAKI SI KUFUNGA WATU

Na Happiness Katabazi
" KATI ya Februali na Juni Mwaka huu, serikali katika kesi za jinai inawakilishwa na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP),  imeweza kushinda jumla ya Kesi za jinai  259 Katika Mahakama zote nne za Mkoa wa Dar Es Salaam na ikajikuta imepoteza ushindi  kesi 76"

Takwimu hizo zimetolewa Jumatano ya wiki hii na Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), Dk.Eliezer Mbuki Feleshi Katika mahojiano Maalum na Tanzania Daima Jumapili,  ofisini kwake  jijiini Dar es Salaam, ambapo anasema  ushindi huo mnono umetokana na utendaji mzuri baina mawakili wa serikali, wapelelezi wa kesi  na mashahidi ambao walifika mahakamani kutoa ushahidi madhubuti ambao mwisho wa siku ulishawsii mahakama hizo kutoa hukumu za kuwatia hatiani washitakiwa na kuwaachilia huru.

Dk.Feleshi ambaye ni mtaalamu wa Sheria za makosa ya jinai, anazitaja Mahakama hizo Kuwa  ni Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar Es Salaam, Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Temeke, Ilala na Kinondoni.

Anasema ofisi ya DPP inaendeshwa kwa mujibu wa Ibara ya 59B ya katiba a Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sheria  ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002 kuanzia kifungu ha 89 . Sheria ya Uendeshaji wa Mashitaka ya Taifa (NPS) ya Mwaka 2008


Anasema  Katika Kipindi Cha Februali  Mwaka huu, Kesi 98 za jinai washitakiwa walitiwa hatiani, Kesi 10 washitakiwa walishindwa Kesi , Kesi 31 zilifutwa,  Kesi Tisa ziliondolewa na  jumla ya Kesi zilizoisha Katika mwezi huo jumla zilikuwa  148.

Aidha Dk.Feleshi  alisema  Katika Kipindi Cha Juni Mwaka huu, Katika Mahakama zote hizo Katika Kesi za za jinai 161 washitakiwa walikuwa wakikabiliwa Katika Kesi hizo 161 walitiwa hatiani, Kesi Tisa washitakiwa waliachiriwa Huru na Mahakama baada ya kushinda Kesi hizo, Kesi 26 zilifutwa na Mahakama, Kesi  mbili  aliziondoa mahakamani baada ya kuona Haja ya kuendelea nayo na hivyo kuwafanya jumla ya Kesi 198 zilizoisha malizika Katika kipini Cha Juni Mwaka huu.

Akianisha idadi hizo za Kesi kila Mahakama zilizofunguliwa na kumalizika, Dk. Feleshi anasema Februali Mwaka huu Katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke,Kesi 36 washitakiwa walitiwa hatiani,  Kesi nne washitakiwa waliachiliwa Huru, Kesi Tisa zilifutwa na jumla ya Kesi 51 zilimalizika Katika Mahakama hiyo ya Temeke.

Kwa upande wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni , serikali ilishinda jumla ya Kesi 37, ikashindwa Kesi Tatu  ambapo washitakiwa waliachiliwa Huru na Mahakama baada ya kuona upande wa jamhuri umeleta ushahidi dhahifu, Kesi 10 zilifutwa, Kesi nne  ziliondolewa na hivyo kufanya jumla ya Kesi 54 kumalizika Katika Mahakama Wilaya ya Kinondoni Katika Kipindi Cha Februali Mwaka huu.

Katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, anasema serikali uliweza kushinda jumla ya Kesi 22, Hakuna mshitakiwa aliyeshitakiwa Kesi , Kesi 12 zilifutwa,na Kesi Moja iliondolewa na hivyo kufanya jumla ya Kesi za jinai 35 kumalizika Katika Kipindi hicho.

Anasema Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar Es Salaam, serikali iliwza kushinda jumla ya Kesi Tatu, Kesi Tatu washitakiwa waliachiliwa Huru , Hakuna Kesi iliyokuwa  na Kesi mbili ziliondolewa na hivyo kufanya jumla ya Kesi nane kumalizika.

Katika Kipindi Cha Juni Mwaka huu, Dk.Feleshi  anasema  Katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke, serikali ilishinda Kesi 45 kwa washitakiwa Kutiwa hatiani, Kesi mbili washitakiwa waliachiliwa huru, Kesi 13 zilifutwa, Kesi mmoja iliondolewa  na hivyo kufanya jumla ya Kesi 61 kumalizika.

" Katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni , upande wa jamhuri ilishinda jumla ya Kesi  30 , ikashindwa Kesi mbili , Kesi Tatu zilifutwa, Kesi Moja iliondolewa na hivyo kufanya Jumla ya Kesi za jinai 36 kumalizika" anasema Dk.Feleshi.

Aidha katika  Mahakama ya Ilala , upande wa jamhuri ilishinda Kesi 71, ikashindwa Kesi nne, Kesi sana zilifutwa na Hakuna Kesi iliyoondolewa na hivyo  kufanya jumla ya Kesi 82 kumalizika na kwamba Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu , upande wa jamhuri ilishinda Kesi 15, ikashindwa Kesi Moja na Kesi Tatu zilifutwa  na Hakuna kesi iliyoondolewa na hivyo kufanya Katika Kipindi Cha Juni Mwaka huu, jumla ya Kesi 198zilimalizika.

' Kwa takwimu hizo hapo ambazo ni za Miezi Miwili tu zinathibitisha wazi kabisa upande wa jamhuri umeweza kushinda idadi kubwa ya Kesi ilizozifungua ambazo ni 259 na imeshindwa Jumla ya Kesi 19 Kati ya Februali na Juni Mwaka huu...sasa Huwa na washangaa sana wale watu ambao Kutwa wamekuwa wakitupoka bila Kuwa na ushahidi Kuwa serikali imekuwa ikishindwa Kesi nyingi mahakamani" anasema Dk.Feleshi.

" Minapenda kuongea na vyombo Vya Habari Kwa kutumia takwimu halisi ambazo zisizo za kupikwa....sasa Hao wanasema Kuwa kila siku upande wa serikali umekuwa  kila kukicha unashindwa Kesi zake mahakamani bila kutoa takwimu uwa nawashangaa sana ., ni kweli kuna baadhi ya Kesi serikali inashindwa lakini wakumbuke Ofisi ya DPP ipo kwaajili ya Kutenda Haki na siyo kutaka mshitakiwa aitwe hatiani hatakama Hakuna ushahidi:

" Ofisi ya DPP, Mahakama unafanyakazi Kwa kutumia vitabu Vya Sheria na siyo hisia na kufuata kelele za watu barabarani wanaotaka serikali Ishinde Kesi bila watu Hao kuisaidia ofisi a DPP Kama kwa Kuwaletea ushahidi mzuri Katika Kesi mbalimbali ili serikali ishinde Kesi. Na Mahakama itamtia  hatiani mshitakiwa baada ya kuridhishwa  na ushahidi na sio kelele za mitaani zinazopigwa na baadhi ya watu wanataka watu watiwe hatiani hata Kama Mahakama inaona haina Haja ya kufanya hivyo" anasema  Dk.Feleshi.

Hata hivyo anasema  ofisi yake HIvi sasa kupitia Kanda zake zote nchini zitaanzisha  utaratibu wa kutoa takwimu za Kuonyesha ni Kesi ngapi serikali ilizifungua mahakamani kwa kila baada ya Miezi mitatu, na serikali ikashindwa Kesi ngapi, imeshinda Kesi ngapi, Kesi ngapi zimeondolewa, na ngapi zimefutwa  ili umma uweze kufahamu ukweli ni upi na mpotoshaji na mwenye Lengo la kupaka Metope serikali Katika Jamii ni nani Kwani HIvi sasa imejengeka tabia ya watu kuzungumza Kuwa serikali imekuwa ikishindwa Kesi nyingi mahakamani bila kutoa takwimu KWA umma Hali inaosababisha umma kuamini  upotoshaji huo.

" Naniachokiona HIvi sasa baadhi ya Kesi ambazo zimekuwa zikiliripotiwa sana na vyombo Vya Habari ikitokea serikali ikishindwa basi baadhi ya watu wanaanza kusema serikali inashindwa Kesi kila siku....ni kweli kuna baadhi ya Kesi ambazo zimekuwa zikivuta hisia za watu Wengi serikali imeshindwa ila kuna Kesi nyingi sana serikali imeshinda ambazo wananchi na Nyie waandishi wa Habari hamzijui na wala hamtaki kuziripoti, serikali imeshinda na rekodi zipo Katika OFISI yangu na Mahakama zote nchini" anasema.
 
Swali: Kwa nini magereza hayaishi
wafungwa?

Jibu: Maana  yake watu kila kukicha wanafungwa.

Swali : Je mshitakiwa kufungwa au kukutwa na hatia na mahakama ni lazima?
Jibu: Hapana  kama ushahidi hautoshi ni haki
ya mtu kuachiwa huru. 

Swali: Je mahakama ni lazima kuendelea na kesi
hata kama kuna kitu kimetatiza?

Jibu: Sio  lazima, mahakama yaweza
kufukuza mashtaka hadi mashahidi wapatikane kama kesi
imekaa muda mrefu bila mashahidi kutokea, hivyo hivyo Jamhuri
inaweza kuiondoa kesi mahakamani pale inapokuwa na sababu
za kufanya hivyo. 

Swali: Je Jaji Mstaafu Mark Bomani  alipowatuhumu mawakili wa serikali siku hizi wamekosa weledi katika tasinia ya uendeshaji wa mashitaka na ndiyo maana serikali hivi sasa imekuwa ikishindwa kesi kila kukicha,alikuwa sahihi?

Jibu: Hapana  wote Jaji Bomani ambaye nae aliwahi Kuwa DPP, aliongea Hilo kwa nadhalia   na vitu vya kufikirika  tu ndiyo maana hakutoa  takwimu japo yupo sawa  kama dhana ni kwamba kila kesi ikienda mahakamani upande wa 
Jamhuri itawalazimisha au kuwashawishi kutoa ushahidi
ilimradi mtu afungwe. 


Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima Jumapili, Julai 27  Mwaka 2014

No comments:

Powered by Blogger.