Header Ads

SAMIA SULUHU HASSAN "STYLE"











Na Happiness Katabazi

SAMIA ni mwanamke wa kwanza kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushika wadhifa wa mgombea mwenza wa Chama hicho Katika mchakato wa kumpata mgombea Urais wa CCM uliomalizika Julai 12 Mwaka huu Mkoani Dodoma ,tangu  CCM ilipozaliwa rasmi Mwaka 1977.

Uteuzi huo ni sifa kubwa kwa sisi Wanawake kwasababu imethibitisha pasiposhaka Kuwa Kumbe wanawake  tunaweza na tu nauwezo.

Pili imethibisha  kile kilio cha wanawake cha muda mrefu cha kutaka wanawake nao wamepewa nafasi za juu za uongozi ndani ya vyama siasa ,serikalini na kwenye taasisi zingine kimesikika kwa kikishindo kwa chama dola CCM kumteua Mwana mama Samia ambaye ni msomi,asiyena na makuu ,mwenye Hekima,Mzalendo,Mzoefu Katika siasa za CCM na ameishapata  fursa ya kushika nafasi ya ubunge katika jimbo la Makunduchi Zanzibar,  Waziri hapa  Tanzania Bara na Zanzibar kupewa nafasi hiyo.

Uchaguzi Mkuu wa taifa letu uliopangwa kufanyika Oktoba Mwaka huu, na CCM ikifanikiwa  kupata ushindi , basi Samia atakuwa  ndiye Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wa kwanza mwanamke tangu Tanzania ipate Uhuru wake Mwaka 1961. Na hivyo ndivyo itakavyokuwa ,tuombe uzima na historia hiyo mpya ya Tanzania Kuwa na Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke itaandikwa Kwenye vitabu Vya Kumbukumbu na Kwenye vichwa Vya watu wanaofikiri Sawasawa.

Binafsi Leo natangaza wazi kupitia ukurasa wangu huu Kuwa Nitamuunga mkono Samia na Patna wake "Bwana Pombe " yaani John Pombe Magufuli ambaye ni Mgombea urais  kwa tiketi ya CCM Katika safari Yao ya " Ukweli" waliyoianza rasmi Julai 12 - Oktba 25 Mwaka huu.

Nawaamasisha  Watanzania wote wanaofikiri Sawasawa Kumuunga mkono Mwana mama Samia Mwanamke  Mtanzania  wa asili ya Zanzibar na Patna wake Bwana Pombe yaani Magufuli.

Nimefanya utafiti wangu nimebaini Samia ni mwanamke anayependa kufunika kichwa chake kwa hijabu,vilemba ikiwemo aina hiyo niliyojitanda Mimi kichwani Katika hii picha yenye sura yangu.

Hivyo kwa wale wanawake wenzangu  ambao  hawana tabia za kuchukia wanawake wenzao pindi wanapoona wanawake wenzao wamefanikiwa kupata madaraka, mali,Fedha siku Moja Moja ikiwa ni Kumuunga mkono mwanamke mwenzetu Samia Katika Safari yake ya Kweli.

Tuwe tunajitanda ushungi wa aina anayependa kujitanda Samia ikiwa ni Ishara ya Kumuunga mkono nakuonyesha Sisi wanawake wa Tanzania Bara,tupo nae sambamba kwasababu Samia ni Mzanzibar na tukifanya hivyo pia kwa njia Moja au nyingine tutakuwa tunauenzi Muungano wetu ambao kwakweli ni wa aina yake licha kuna Mahasidi wachache wanataka Muungano Uvunjike na Hilo haliwezekani.

Mungu Ibariki Tanzania

Chanzo: Blogg: www.katabazippy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
22/7/2015.

No comments:

Powered by Blogger.