Header Ads

ASKARI SHUPAVU LAZIMA APITE DEPO



* WALINZI WA LIPUMBA HAWAKUPITA DEPO NDIYO MAANA SIYO SHUPAVU 

Na Happiness Katabazi
WALINZI  wa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba siyo Askari  shupavu kwasababu hawajapita Depo na Lipumba ona haja sasa ya kuajiri walinzi wengine wapya ambao wana Mafunzo na mbinu za kisasa za Kupambana na maadui wako. 

Haiingii akilini Mlinzi wa kiongozi mkubwa kama Lipumba anakubali kudhibiti wa kirahisi  namna   ile na polisi halafu kufurukuta kidogo mbele ya wanaume wenzio 'polisi' ushindwe.

Bora Lipumba uniajiri Mimi niwe mlinzi wako Kwani kwa video hii ni wazi Huna walinzi imara na ipo siku watakuja kukutelekeza kwenye Majanga Kama ya aina hiyo ili wazinusuru nafasi zao.

Tunaambiwa Kuwa mlinzi anayemlinda kiongozi yupo Tayari kufa yeye kwanza  ili kuakikisha anamnusuru kiongozi anakuwa salama Katika balaa lolote. Profesa Lipumba au walinzi wako Hao ni Makorokoroni?

Video hii ,Polisi wameweza kuwazingira  na kuwatandika kirahisi na kumchukua kiraini  Boss wao Lipumba ambaye Lipumba wakati akiwa mikononi   mwa wanaume 'Polisi' alionekana Kuwa mpole sana na nidhamu ya hali ya juu utafikiri siyo Lipumba huyu tunayemfahamu ambaye awapo majukwaani na Katika mikutano ya waandishi wa Habari uwa anajifanya mwanaume  Jabari wa kuongea na Kumea mambo utafikiri anaweza kurusha ngumi,Kumbe wapi.

Binafsi wakati mwingine uwa na wanazarau sana wanaume wanapenda sana kuongeaongea sana huku mitaani na kujifanya wenyewe ni wanaume washoka hawaogopi kitu.

Kwasababu wanaume Wengi wa Ana hiyo nimewashuhudia sana wakifikishwa mahakamani,Polisi au wakiwa magerezani kwakweli wanakuwa na nidhamu ya Hali ya juu, Isipokuwa Swaiba wangu Mchungaji Christopher Mtikila ,huyu ni mwanaume wa Shoka na Nina mkubali sana Kwani hata akiwa mikononi mwa Polisi,Magereza yeye ujasiri wake upo pale pale na kidogooo pia 'mume wangu wa zamani', Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Agustine Mrema.

Wito wangu kwa wananchi Tusikubali kushiriki maandamano yanayovunja Sheria za nchi ambayo yamekatazwa mwisho wa siku mtaishia kula kisago na  Fedha za kujitinia majeraha ni tabu kupata, Mwenzenu Lipumba Jana kaugua kidogo Maradhi ya moyo kukimbizwa haraka Hospitali ya mAana kutibiwa, Nyie Maskini wenzangu nani aliwapatia Fedha ya kwenda kujitibia  majeraha?

By Happiness Katabazi
Januari 29 Mwaka 2015.

No comments:

Powered by Blogger.