Header Ads

KATABAZI: NIMEACHA KAZI GAZETI LA TANZANIA DAIMA



KATABAZI : NIMEACHA  KAZI GAZETI LA TANZANIA DAIMA
: KWASASA NI OFISA  HABARI CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO(UB)

MIMI  Happiness Thadeo Katabazi (35), Leo Agosti 29 mwaka 2014 ndiyo siku yangu ya mwisho ya kufanyakazi Katika Gazeti la Tanzania Daima.

Nimeachakazi kwa Hiari yangu    katika Gazeti la Tanzania Daima linalotolewa na kampuni ya Free Media  Ltd  kwasababu Agosti  Mosi Mwaka huu,niliwasilisha notisi ya kuacha Kazi   na ombi  hilo lilikubaliwa na waliokuwa wakubwa wangu  wa Kazi.

Kwa heshima na taadhima napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu Kwani alinipa Afya,Nguvu na maarifa nikaweza kulitumikia Gazeti la Tanzania Daima kwa Miaka nane sasa  kwa uaminifu na uadilifu wa Hali ya juu.

Kwasababu kwa Kipindi chote nilichofanya Kazi Kama Mwandishi wa Habari wa Gazeti Hilo sijawahi kuandika habari ambayo ilisababisha gazeti Hilo lifnguliwe kesi mahakamani.Namshukuru Mungu Katika Hilo.

Pia namshukuru mmiliki wa Gazeti la Tanzania kwani bila yeye kuanzisha Gazeti Hilo nisingepata ajira na limenilea.  Napenda kuwashukuru wafanyakazi wote wa gazeti hilo kwani tuliweza kufanyakazi pamoja licha wakati mwingine ilikuwa ikitokea Hali ya kutofautiana misimamo Katika baadhi ya mambo mbalimbali lakini yaliyopita Si ndwele tugange yajayo.

Navishukuru   vyombo vyote vya dola likiwemo Jeshi la JWTZ,Polisi, Magereza, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kwani baadhi ya maofisa wa vyombo hivyo walikuwa wakinipa  ushirikiano wa kutosha Katika Kazi yangu ya uandishi wa Habari za mahakamani kwa Miaka 16 sasa. 

Nimevitaja vyombo hivyo Vya dola Kwani Mwandishi makini na mjanja wa  Habari za mahakamani nilazima afanyekazi kwa kutegemea Polisi, Askari Magereza na TAKUKURU.

Nawashukuru sana Askari na maofisa wote wa majeshi hayo Kwani tulifanyakazi  pamoja na nilijifunza mambo mengi sana kutoka kwenu.Mungu awabariki na nitaendelea kuthamini mchango wenu Kwangu Kwani mlinifundisha  mengi hasa Askari wa Jeshi la Polisi " Manjagu".

Navishukuru vyama Vya siasa Chama Cha Malpinduzi( CCM), CUF, NCCR- Mageuzi , CHADEMA, Tanzania Labour Party , DP na vingine Kwani katika Kipindi chote Cha Kazi yangu ya uandishi wa Habari niliweza kufanya Navyo Kazi kupitia viongozi wa juu,Kati na wanachama wa vyama hivyo.

Kwa namna ya kipekee  napenda kuishukuru  Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), iliyokuwa ikiongozwa na DPP aliyemaliza muda wake hivi karibuni, Jaji DK.Eliezer Feleshi Kwani ni yeye Jaji Feleshi  na timu yake ya Mawakili wa serikali walikuwa wakinipa ushirikiano Katika Kazi yangu ya uandishi wa Habari za mahakamani kwa Miaka Saba yote aliyokuwa ameshika wadhifa   huo wa DPP.

Namshukuru sana Jaji Feleshi Mungu ampe Maisha Marefu Kwani Jaji Feleshi yeye binafsi alikuwa na hadi sasa ni  Mpenzi  wa makala na Habari zangu za mahakamani na nimshauri mkubwa sana wa mambo yangu binafsi,kazi na shule yangu. Feleshi mimi namchukulia kama ni kaka yangu, mwalimu na mshauri wangu wa kazi yangu ya uandishishi wa habari, na kozi yangu ya Sheria.

Jaji Feleshi amekuwa akinikosoa ninapoandika  Habari au makala ambazo alikuwa akiziona hazikidhi matakwa ya kisheria na usalama wangu binafsi na nchi.

Na hadi sasa ajachoka kunishauri na amekuwa akinitaka kabla ya kuandika niwenafanya utafiti kwanza na kweli ushauri wake nimeuzingatia kwani hivi sasa amekuwa akiniambia sasa anaona fahari kwani uandishi wa makala zangu umebadilika imetoka Katika ngazi ya kiharakati , Ujinga na umemfika ngazi ya Kisomi.Namshukuru sana Jaji Feleshi 'Msukuma'.

Naushukuru uongozi wa Mhimili  wa Mahakama nchini chini Jaji Mkuu Mstaafu, Agustino Ramadhani na Jaji Mkuu wa sasa Mohamed Chande Othman kwasababu kuna baadhi ya Majaji, wasajili,makarani, walinzi wa Mahakama na watumishi wa Kada mbalimbali wa  Mahakama walinipa ushirikiano na kunifundisha mambo mbalimbali ya jinsi mahakama na serikali inafanyaje kazi bila kuchoka wakati nilipokuwa Mwandishi wa habari za mahakamani bila kuchoka.

Pia navishukuru Vyanzo Vyangu vingine Vya Habari ambavyo ni Mawakili wa kujitegemea,walalamikaji, washitakiwa waliopo nje kwa dhamana na waliopo ndani ya magereza walikuwa wakinipa taarifa mbalimbali kuhusu Kesi mbalimbali na kuaniarifu mapema Kuwa siku Fulani mahabusu waliopo Katika baadhi ya magereza watagoma lini , nawashukuru sana na taarifa hizo nilikuwa nazifikisha mahali husika zinafanyiwa Kazi.

Hata hivyo nayashukuru  makundi mengine yote yaliyokuwa yakinipa ushirikiano Katika Utendaji wangu wa Kazi.

 Pia na washukuru wasomaji na wapenzi wa makala zangu na Habari za mahakamani Kwani kwa Kipindi chote hicho mlikuwa mkisoma makala na Habari zangu wengine mlikuwa mkinipinga na wengine mlikuwa mkiniunga mkono.

Licha ya kuacha Kazi Gazeti la Tanzania Daima, napenda Kusema wazi  Kuwa Kazi ya uandishi wa Habari hasa uandishi wa Habari za mahakamani ' umbea' ipo Kwenye Damu yangu, nitaendelea kuandika makala na kuchangia mijadala tofauti kupitia mitandao ya kijamii bila kuvunja Sheria za nchi.

Kwa sasa nimepata Kazi Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB) na Makamu Mkuu wa Chuo hicho ni Profesa Balozi Costa Ricky Mahalu, chenye Makao Makuu Mikocheni  kwa Warioba Dar es Salaam, Kama Afisa Habari wa Chuo Kikuu hicho. 

Nawakaribisha waandishi wa Habari wenzangu hasa wale waandishi wa Habari za mahakamani na wananchi wengine  waje UB, ili waweze kupata elimu za  fani mbalimbali maana Ulimwengu wa sasa bila elimu ni tabu sana.

Waandishi wa Habari tukiitikia wito wa kukubali kwenda kujiendeleza kielimu Katika vyuo vikuu, ni wazi tutaondokana na tabia ya kukubali kutumiwa vibaya na Makundi yanayoasimiana kisiasa, Kibiashara kuchafua watu kupitia Karamu zetu, kujazana Ujinga ndani ya  vyumba Vya Habari .

Nafahamu neno Hilo linaweza kuwakera baadhi ya waandishi ambao hawataki  Mabadiliko na hawataki kujiendeleza kielimu kwasababu za kijinga Kuwa akienda shule kusoma Atakosa ' mishiko, safari'.Sijali, naamini nimesema kweli na Mungu atanilinda  na inawezekana ukiamua.

Mimi ni shahidi wa Hilo Kwani Mwaka 2009 -2010 nilipoanza kusoma kozi ya Cheti Cha Sheria Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, kuna baadhi ya waandishi wenzangu walinicheka na kuniona chizi lakini nikamaliza Mwaka 2012- Juni 2013 nikasoma Diploma ya Sheria Katika Chuo Kikuu Cha Bagamoyo nikamaliza waliokuwa wananicheka Wakaanza kuniambia Kuwa walifikiri nilikuwa natania wakati nawaaga na kwenda Kusoma Sheria.

Waliposikia na kuniona Septemba  Mwaka 2013  nimeanza kusoma Shahada ya Sheria wameishia  Kusema Kuwa Kumbe nimedhamiria, na kwamba Mimi ni mwanamke wa Shoka na kwamba nitafika Mbali.

Nawatazama   kwasababu hawafahamu nawaza nini na ni kwanini MUNgu ananipa Nguvu na uwezo wa kusoma hivyo wakati Nasoma kwa tabu sana na kugeuka ombaomba wa Ada" Matonya'.

Licha Nasoma shule kwa dhiki na tabu lakini siku zinakwenda na shule ndiyo MUNgu akipenda  Julai Mwaka 2016 nitamaliza Shahada  ya kwanza ya Sheria.

Nimelazimika kujitolea mfano halisi Mimi licha sikupaswa kutaja adharani Kuwa Nasoma Kwa  dhiki, ili iwe ni amasa kwa wanahabari wenzangu ambao hawana mawazo kabisa ya kujiendeleza kielimu  Kuwa ukiamua na ukamtanguliza Mungu  inawezekana.

Mume wangu 'Rais Mdhurumiwa' Marehemu Dk.Sengondo Mvungi, Profesa Paramaganda Kabudi,Dk.Harrison Mwakyembe, Mwanangu ambaye ni mtoto wa mume wangu Marehemu Dk.Mvungi, ambaye ni Mkuuu wa Kitivo cha Sheria (UB) na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Dk.Natujwa Mvungi hawa wote walikuwa ni waandishi wa Habari.

Tena  bora na DK. Mwakyembe na Dk.Natujwa walisomea  kozi ya uandishi wa Habari lakini  marehemu Dk.Sengondo Mvungi hakuwahi kusomea chuo chote kozi ya uandishi wa Habari licha alikuwa ni Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mzalendo na Dk.Mvungi alipelekwa kufanyakazi Gazeti la Mzalendo na Mwandishi Mkongwe nchini, Ndimara TIgambwage.

Lakini mwisho wa siku waliamua kukata shauri na kwenda vyuoni Vya elimu ya juu kusoma  fani ya Sheria na Leo hii wamekuwa ni msaada mkubwa kwa taifa hili Kwani wamekuwa wAkitumiwa na serikali, Jamii kutoa huduma ya taaluma Yao ya Sheria.

Hivyo binafsi nikiwa Natazama historia za  wasomi hawa, nimejifunza   jambo Moja Kuwa ukiamua kukata shauri kutaka kujiendeleza kielimu unaweza. Waandishi wenzangu ambao bado hamjakata shauri , hamjachelewa, anzeni sasa.

 Swahiba wangu Mchungaji  Christopher Mtikila tukutanapo au tupigianapo simu neno la lake la kwanza kuniambia ni "Saa ya Ukombozi...Mimi na Mjibu ni Sasa". 

Mataifa ya wenzetu yamepiga Hatua za kimaendeleo kwasababu waandishi wao wa Habari wameweza kwenda shule vizuri na Waandishi wao wengine wameamua kubobea Katika Nyanja Fulani , mfano Mwandishi wa Habari za mazingira amesomea kozi ya mazingira hivyo akiandika Habari inayohusu mazingira anaifahamu vizuri kwasababu.

Kama kweli waandishi wa Habari wa Tanzania tumedhamilia kulilitetea taifa letu maendeleo, basi tuzidi kujiendeleza kielimu na ikiwezekana tusomee fani nyingi tofauti na uandishi wa Habari ili mwisho wa siku uakiamu kuandika makala au Habari inayohusu labda mambo ya uchumi, Afya , Sheria unaiandika vizuri tena bila msaada wa Wanataaluma ya ya uchumi, Sheria au Afya kwasababu Tayari unakuwa unafahamu nini unachokiandika kwa mujibu wa taaluma hiyo.

Naamini tukiamua kujiendeleza kielimu miongoni mwenu 'mtakataa kugeuzwa geuzwa Kama  chapati'  na baadhi ya wanasiasa na Makundi mengine yenye Fedha ambayo ya natumia Fedha zao kuwahonga baadhi ya waandishi wa Habari kuchapisha Habari ambazo hazikidhi vigezo na zenye Lengo la kuchafua watu wengine.

Mwisho Nawashukuru wale wote walionishauri niende kusoma Sheria Kwani Leo hii naona faida ya ushauri wao kwani nimeweza kupanuka kifikra na kuwa imara katika fani yangu ya uandishi wa habari.Mungu awabariki sana.
Imeandaliwa na ; 
Happiness  Katabazi
Ofisa  Habari wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB),
Mwanafunzi wa Mwaka wa pili wa Shahada ya Sheria(UB)
0716 774494.
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Agosti 29 Mwaka 2014

No comments:

Powered by Blogger.