Header Ads

KUJADILI MUUNGANO ISIWE DHAMBI , USALITI




Na Happiness Katabazi
KADRI siku zinavyozidi kusonga mbele, ile  kasumba ya kumhesabu mtu yeyote  anayekosoa jambo lolote linalousu upande mmoja wa Muungano wa Zanzibar na Tanzania Bara Kuwa ni msaliti,anataka kuuvunja Muungano huo, inaanza kupoteza Nguvu.

Pia ile Hali ya woga waliyokuwa nayo Watanzania Bara Wengi yakuogopa kujitokeza adharani kutoa hoja zinazokosoa baadhi ya mapungufu ya nayo fanya au yaliyofanywa  na baadhi ya wazanzibari au serikali yake,au baadhi ya manufaa wanayoyapata Wazanzibar Katika Muungano, Kwa kisingizio Cha Kuogopa kutolewa lugha chafu toka Kwa baadhi ya wanasiasa wa Zanzibar ,unatoweka kwa kasi ya ajabu.

Nasema hivyo Kwasababu miaka ya nyuma ilidaiwa  Kuwa kuna baadhi ya wanasiasa   (Majina ninayo),  Kuwa waliwahi kushughulikiwa kimya kimya tena kikamilifu  na vyama vyao kwa kisingizio tu wanasiasa  Hao walikuwa wanapinga Muungano.

Lakini kwa mujibu wa baadhi ya wanasiasa hao  ambao niliwahi kupata fursa ya kuzungumza  nao ana kwa ana wengine kupitia Kwa watu wangu wa karibu,  hawakuwahi kufikiria kuvunja Muungano, isipokuwa walikuwa na mtazamo tofauti kuhusu baadhi ya mambo ndani ya Muungano na walikuwa wanataka  yarekebishwe kwa njia ya Amani.

Kumbe Mitazamo hiyo ilichukuliwa vibaya na Waliokuwa na madaraka Kipindi hicho, wakatumia njia zao kuwashughulikia watu Hao kikamilifu.

Lakini Kwa baadhi ya wanasisasa  hawakuwa na nia Mbaya na ukweli siku zote utasimama, Leo hii Tunaona  baadhi ya wanasiasa waliosurubiwa kule Zanzibar kimya kimya Kwa fitna eti ni Wapinga Muungano,Leo hii Mungu  amewajalia ameruhusu wamepewa madaraka makubwa ndani ya Serikali ya Zanzibar na Tanzania Bara na ule uongo Waliokuwa wamepakaziwa Kuwa ni Wapinga Muungano na endapo wa wakipewa madaraka watavunja Muungano, sijui zimezikwa Katika makaburi gani.

Mei 27 Mwaka huu,ni baadhi ya ni kielelezo cha   hayo niliyoyasema hapo juu,Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally  Kessy aliwashambulia  Wazanzibar, kwamba hawana sababu ya kulalamikia kutaka haki sawa kwenye kila jambo la muungano wakati hawachangii kitu kwenye Serikali ya Muungano.

 Mbunge huyo aliyeamua kujilipua , alitoa kauli hiyo ndani ya Bunge, wakati akichangia hoja ya hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka wa fedha 2014/2015, inayoongozwa na Waziri  Bernad Membe.

Kessy alichangia hoja hiyo akijibu hoja ya Kambi Rasmi ya Upinzani iliyosema kuna upendeleo mkubwa na uwiano usio sawa kati ya Tanzania Bara na Visiwani katika uteuzi wa mabalozi wa Tanzania nje ya nchi.

Kessy  alisema kwa zaidi ya miaka 20 , Zanzibar, haichangii kitu katika Serikali ya Muungano, lakini ndio vinara wa Kulalamika  na kutaka usawa kwenye kila jambo., Kauli iliyozua zogo Kwa dakika zisizopungua tano.

Wakati  akiendelea kuchangia hoja hiyo, Mbunge wa Chakechake, Mussa Haji Kombo (CUF), aliomba mwongozo wa Naibu Spika dhidi ya kauli hiyo.

“Mheshimiwa Spika, kuna mwendawazimu mwingine ni mtu anayepiga piga mawe hovyo, mwingine anakuwa mtu wa kuchekacheka, akipita anaweza kuwa anacheka tu ‘kwekwekwe’, na mwendwazimu mwingine ni yule anayeongea ovyo  mbele ya watu wenye heshima zao kama tulivyo humu ndani.

Baada ya Naibu Spika Job Ndugai kuarisha Bunge , imeelezwa kuwa wabunge kutoka Zanzibar waliwahi kutoka nje kumkabili Kessy. Mbunge wa Magogoni, Kombo Khamis Kombo, Sanya Mohammed Sanya na wabunge wengine wa CUF, walimzonga Kessy, kutaka kumpiga.

Kama si uwepo wa baadhi ya wabunge wa CCM walioamua kumuweka kati Kessy, mbunge huyo angepigwa na wabunge kutoka Zanzibar ambao walionyesha dhahiri kukerwa na kauli zake.

Ibara ya 17 (1) Cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 , inasomeka HIvi: " Kila raia wa Jamhuri  ya Muungano anayo Haki ya kwenda  kokote  katika Jamhuri ya Muungano  na kuishi  Katika sehemu  yoyote, kutoka  nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa  Kuhama au kufukuzwa  kutoka  Katika Jamhuri ya Muungano.

Sasa kwa mujibu wa Ibara hiyo, tu muulize huyu Mbunge wa Magogoni , Kombo Khamis Kombo, amepata wapi madaraka ya kutaka Kessy azuiwe kwenda Zanzibar? 

HIvi tukisema Kombo Ndie Kinara wa UBaguzi na amevunja  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977  ya Kutaka Kessy asiruhusiwe kwenda Zanzibar, tutakuwa tumekosea?

 Wale wabunge wa Zanzibar walipaswa watuambie tena kwa njia ya Amani na kuongea bila Ruhusu  ya Spika Ndugai mithili ya watu walipandisha mashetani, Kuwa  Kessy alisema uongo, siyo kwa vitendo vile Vya kiuni walivyovifanya ndani ya Bunge Kwa Kuzua  tafrani  ndani ya bunge na nje ya Bunge bila kufuata Taratibu wakati wao ni Watunga Sheria.

Minamuunga mkono Kessy kwamba baadhi ya Wanzanzibar kwasababu wanazozijua wao wamekuwa vinara wakulalamika  kila kukicha kwamba Wanzanzibar wanaonewa , Mara Muungano uvunjwe,wananyonywa  sana na Tanzania Bara na hawaoni faida ya Muungano na kwamba wabaya tuwaachie Zanzibar Yao.

Sasa kosa la Kessy hapa liko wapi hadi wabunge Hao wazanzibari wamsonge vile?  Kessy amesema ukweli Kuwa ni kweli baadhi ya wazanzibar wamekuwa ni vinara wakilalamika na kutaka uwiano sawa Katika kila jambo la Muungano wakati Zanzibar inachangia kidogo.

Kwani  si kweli Tanzania Bara inachangia pato kubwa Katika Muungano kuliko Zanzibar?Shida inatoka wapi ? Mbona nafasi nyingi za uongozi huko Zanzibar zimeshikwa na wazanzibar Mbona Watanzania Bara hawalalamiki Katika Hilo?

Napata wasiwasi Kuwa uenda wale wabunge waliozua tafrani uenda walikuwa na ajenda Yao nyingine wakasingizia Kessy amewakara.  Maana haiingii akili ni kabisa kilichosemwa na Kessy Ndio kiwapandishe jazba na kutaka kumpiga wakati Kessy aliyoyasema siyo  mambo mapya  na wabunge  hao walishindwa kutoa vielelezo  vinaonyesha  kuwa Kessy aliyosema ni ya  uongo.

Kessy amekuwa jasiri Kati ya wanasiasa wachache wa Tanzania Bara ambao Wengi wao wamekuwa na mtazamo sawa Kama wa Kessy, lakini wamekuwa wakisemea  chini chini  kwa  kisingizio Kuwa wanaogopa kutolewa lugha chafu kutoka kwa  baadhi ya wazanzibar na kuambiwa Kuwa wanataka kuvunja muungano.

Ndio mAana Katika hili Nampongeza Kessy kwa ujasiri  wake wa kulisema Hilo adharani. Na ieleweke wazi tamko Hilo la Kessy Kwa watu wenye akili timamu hawawezi kuona Kauli hiyo ya Kessy it's sababisha   Muungano wetu ambao ni wa mfano  wa kuigwa , ukavunjika au tukasema Kauli hiyo inaashiria kuwabagua Wanzanibar. 

Siku zote Spika Anna Makinda awapo Bungeni amekuwa aliwakumbusha wabunge Kuwa mambo yanayo jadiliwa ndani ya Bunge yaishie ndani ya Bunge,wabunge Hao wajiende kuyajadili nje ya Bunge?

Tuwaulize Hao baadhi ya wabunge toka Zanzibar ambao imeelezwa Kuwa Muda  mfupi baada ya Spika Ndugai kuairisha  Bunge mchana , Mei 27 Mwaka huu, mchana baada ya Muda  mfupi mvutano huo baina wabunge wazanzibari na Kessy Kuibuka ,kumvizia Nje ya Bunge na kuanza kumzonga Kessy, hawaoni walikuwa wanajidhalilisha na kujishushis  heshima zao Mbele ya watu wenye akili timamu na wanao wafahamu na kupuuza agizo Hilo la Makinda?

Kama siyo nongwa na kama gubu la mke mwenza Ni kitu gani? .Jambo limetokea Ndani ya Bunge, Spika Ndugai  akalitolea msimamo ,kwanini wabunge Hao wazanzibari waende laze jambo Hilo nje ya Bunge Kama siyo Nongwa kitu gani?

Hivi Zanzibar na wazanzibari siku hizi wamegeuka Kuwa miungu watu hadi Hawataki wasemwe au wakosorewea? MAana Mifano siyakutafuta, ukisema adharani Zanzibar siyo nchi....utajuta kuzaliwa wakati  Ibara ya 1 ya Katiba ya nchi inasema hivi: " Tanzania ni nchi moja  na ni Jamhuri ya Muungano".

Na Ibara ya 2 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasomeka hivi: " Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote  la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya Bahari Tanzania inapakana nayo."

Lakini kuna baadhi ya wanasiasa uchwara toka Zanzibar kwa sababu wanazozijua wamekuwa wakipotosha ukweli huo kwa kusema Zanzibar ni nchi.Na tungali tukikumbuka Yaliyomkuta Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye ni msomi wa sheria kutoka kwa baadhi ya wabunge wa siasa kwa hatua yake ya kusema kuwa Zanzibar siyo nchi.

Wasomi wa Sheria tunafahamu Kuwa Zanzibar siyo nchi kwasababu ina kosa sifa ya kutokuwa na huwezo wa kuingia mikataba na mataifa ya nje , haina jeshi, haina sarafu yake .

Na  mwanafunzi wa Sheria akipewa  swali Katika mitihani akiulizwa  Kuwa Zanzibar ni nchi au siyo Nchi, akijibu   Zanzibar ni nchi, basi mwanafunzi Huyo akae akijua amekosa.

Sasa kinachonisikitisha  ni hawa wanasiasa uchwara ambao wanapotosha umma kwa makusudi kwakusema Zanzibar ni nchi kamili wakati si kweli.Tabia hiyo ikome.

Kessy alivyokuwa   akichangia hoja yake Bungeni wiki hii, Alisema   Kwa  zaidi ya Miaka 20 , Zanzibar haichangii Muungano yaliyompata wote ni mashahidi. Mbona hata Kazi iliyofanywa na Mungu ya  uumbaji inasahihishwa na binadamu?

 Mfano Leo hii mwanaume ananibadilishia jinsia yake, wanawake wenye rangi nyeusi wanajipaka mikorogo mikali na Kumeza madawa ili wawe weupe na baadhi ya wanawake wenye Matiti madogo wanaenda mahospitali Makubwa kufanyiwa upasuaji ili wawe na Matiti Makubwa.Wengine wanameza madawa kuongoza ukubwa wa jinsia ya Kiume.

Sasa Kama baadhi ya binadamu tumefika Hatua ya kukosoa Kazi ya Mungu wetu na wala mungu  hapigi  kelele wala kutukana watu,anajua atatuadhibu Kwa  njia gani, kwanini Nyie baadhi ya wazanzibari mnapokosolewa mnatoa lugha chafu, mnataka Kessy asiruhusiwe Kuja Zanzibar? 

Kwani Zanzibar ni Mbinguni au peponi  hadi Kessy akizuiliwa Kuja huko ndiyo itabidi aende Kwenye Moto  wa milele Jehanamu?

Wabunge wetu jifunzeni Kujenga hoja Kwa vielelezo na mjenge  utamaduni wa Kupenda kujisomea  , siyo Kujibu  hoja ya mbunge mwenzio kwa kutumia lugha zisizojulikana na  stahaa, vitisho.

Haisaidii Kwani zaidi ninachokiona Kwa  Mwenendo huo Bunge linatuaribia watoto na Jamii Kwa  ujumla Kwa lugha chafu na vitendo Vya kihuni vinavyofanywa na baadhi ya wabunge ambao Jukumu la kufikiri wamelibinafsisha  na hawataki  kufikiri na kufanya utafiti Kabla ya kujadili mada mbalimbali.

Nasisitiza tena kuwa naupenda Muungano na sipendi Muungano huu uvunjike bila Sababu zisizo na Msingi, ila nilazima wazanzibari Wakubali Kuwa Zanzibar  ni ndogo ukilinganisha na ardhi ya Tanzania Bara pia Hakuna ubishi Kuwa idadi ya wanzanzibar ni ndogo ukilinganisha na Watanzania Bara .

Nawapenda  Wazanzibari , sina  chuki nao na wengine ni marafiki zangu wa karibu na tunaishi vizuri .Na siyo wazanzibar wote ni wakorofi, ni wachache wakorofi ambao ni wanasiasa na wengine wanatumiwa na wanasiasa wenye uchu wa madaraka na wasioutaka Muungano kuleta Chokochoko, na wasivumiliwe watu hawa.

Nimalizie Kwa Kusema kuwa Katika hili Nampongeza  Kessy kwa Ushujaa wake wa Kusema hayo aliyoyasema adharani bila kujificha na alichokisema kuhusu Baadhi ya wazanzibari ni kweli tupu na wala siyo ugomvi,  Kwani kuna watu wanazungumzia hayo aliyoyasema Kessy vichochoroni kwa kisingizio cha Kuogopa kutukanwa na baadhi ya Wazanzibari. 

Kilichofanywa na baadhi ya wabunge kutoka Zanzibar siku hiyo Kwa kisingizio eti Kessy ametoa Kauli ya kuwabagua wazanzibar, ni Cha kiuni na hakikustahili kufanywa na wabunge Hao ambao waliaminiwa na wananchi wao wakawapiga kura lakini Matokeo yake wabunge Hao mapema wiki hii wamejigeuza wahuni wa mitaani na kufanya vitendo vile Vya kihuni.

Mhuni, na watu wasiyojiheshimu   ndiyo wanaofanya vitendo Kama vile lakini Kamwe MTu anayejiheshimu ,Anastaa,  uvumilivu wa kisiasa hawezi kufanya uhuni ule uliofanywa na baadhi ya wabunge wazanzibar. Huo ndiyo ukweli, jirekebisheni, na Muungano wetu unaendelea kudumu na wanaotaka kuuvuruga kwa maslahi Yao binafsi washughulikiwe.

Tuendelee kudumisha Muungano wetu.


Chanzo: Gazeti  la Tanzania Daima la Jumapili ,Juni Mosi Mwaka 2014.












No comments:

Powered by Blogger.